Mbarawa akoshwa naTPA ujenzi wa bandari mpya ya Mbamba Bay

Waziri wa Uchukuzi Mheshimiwa Makame Mbarawa ameisifu Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA) kwa utekelezaji wa ujenzi wa bandari mpya na ya kisasa ya Mbamba Bay inayojengwa pembezoni mwa Ziwa Nyasa katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma; akisema kuwa ujenzi huo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuboresha bandari mbalimbali hapa nchini. Akizungumza…

Read More

Profesa Mkumbo ataka uwekezaji zaidi viwandani

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema uwekezaji katika viwanda ndio msingi wa kukuza uchumi. Profesa Mkumbo amesisitiza kuwa maendeleo ya nchi yeyote huonekana katika uwekezaji na katu hakuna nchi duniani iliyoendelea bila uwekezaji. Waziri huyo ametoa kauli hiyo jana Septemba 18, 2024 wakati akizindua ukumbi…

Read More

Mwakilishi ahoji fidia kwa waliopisha miradi ya umeme

Unguja. Wakati mwakilishi wa Mtambwe, Dk Mohammed Ali Suleiman akiwasilisha kilio cha wananchi waliopisha miradi ya umeme bila kulipwa fidia, Serikali imekiri kuwapo changamoto hiyo na kueleza hatua inazochukua ili kuwalipa. Dk Suleiman ametoa malalamiko hayo leo Septemba 19, 2024 kwenye Baraza la Wawakilishi, huku akiipongeza Serikali kwa kufanikisha miradi ya umeme. Hata hivyo, amesema…

Read More

Hapatoshi maandamano ya Chadema, wadau wacharuana

Dar es Salaam. Kufuatia hali ya sintofahamu ya demokrasia nchini, baadhi ya wadau wa siasa na demokrasia wametaka kuwepo kwa mazungumzo ya kutafuta mwafaka miongoni mwa vyama vya siasa. Mazungumzo hayo yameshauriwa yafanyike ili kurejesha hali ya maridhiano katika kipindi ambacho Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamepanga kufanya maandamano Jumatatu ya Septemba 23, 2024….

Read More

Nahodha JKT amkingia kifua Ateba

NYOTA wa JKT Tanzania, Edward Songo amesema moja ya usajili wa wachezaji wa kigeni waliomvutia msimu huu hadi sasa ni mshambuliaji wa Simba raia wa Cameroon, Leonel Ateba aliyejiunga nao akitokea USM Alger ya Algeria. Songo aliyewahi kutwaa tuzo ya mchezaji na mfungaji bora wa Ligi ya Championship msimu wa 2022-2023 akiwa na timu hiyo…

Read More