‘Hospitali’ ya Cradle yafikishwa kortini madai kifo cha pacha wa kupandikizwa
Dar es Salaam. Kituo cha Afya cha Cradle (Cradle Speciality Heath Centre), kilichopo Msasani, jijini Dar es Salaam kimeburuzwa mahakamani kikidaiwa fidia ya zaidi ya Sh3.6 bilioni kwa madai ya uzembe uliosababisha kifo cha mmoja wa watoto pacha waliozaliwa hapo kwa njia ya upasuaji. Kesi hiyo imefunguliwa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam na Julieth Baigana…