Kamisheni ya Ardhi yalalamikiwa ucheleweshaji wa hatimiliki

Unguja. Baadhi ya wananchi wameiomba Kamisheni ya Ardhi kubadilika kutokana na mzunguko mrefu uliopo kwa watu wanaotafuta hatimiliki za ardhi za kilimo. Akizungumza leo Septemba 18, 2024 katika uzinduzi wa utoaji hati hizo, Aziza Ibrahim Ahmed, mkazi wa Kwa Goa amesema ni mwaka wa sita sasa amekuwa akihangaika kutafuta hati hiyo. Amesema alikata tamaa ya…

Read More

Tanzania, Mali kriketi bato la historia

TANZANA  inaikaribisha Mali katika mchezo wa kihistoria wa ufunguzi wa michuano ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia za kriketi ya mizunguko 20 keshokutwa, Dar es Salaam. Ni mchezo unaoikaribisha Mali, nchi iliyotawalia na Wafaransa katika mchezo unaochezwa zaidi na nchi za Jumuiya ya Madola ambazo huzungumza Kiingereza. Mali inajiunga na Msumbiji nchi inayoongea Kireno ambayo …

Read More

Waziri Bashe azungumza na wakulima kituo cha ununuzi wa mahindi Kizuka, Ruvuma

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, amefanya ziara ya ukaguzi katika Kituo cha Ununuzi wa Mahindi cha Kizuka, mkoani Ruvuma, Septemba 18, 2024, ambapo alikutana na wakulima waliokuwa wakichekecha na kuchambua mahindi. Akiwa katika ziara hiyo, Waziri Bashe alisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imejipanga kutatua changamoto za wakulima kabla…

Read More

Madrid kufanya kufuru mpyaa! | Mwanaspoti

MOTO wa Real Madrid hii unatosha au hautoshi? Basi kabla hujafikiria chochote, miamba hiyo ya Bernabeu, huenda ikawa kwenye mwonekano tofauti kabisa wa Galacticos mpya msimu ujao. Miamba hiyo ya Hispania imetumia miaka mitano kujikusanya na kujiweka pazuri kifedha na sasa ipo tayari kuanza kutumia kwa kuleta mastaa wa maana kabisa kwenye kikosi chao kwa…

Read More

Tanzania yafanikiwa Kuzuia Asilimia 86 ya Uzalishaji wa Kemikali Hatari kwa Tabaka la Ozoni – MWANAHARAKATI MZALENDO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Ashatu Kijaji amesema Tanzania imefanikiwa kuzuia tani 216 sawa na asilimia 86 ya uzalishaji wa kemikali hatari kwa tabaka la ozoni ambazo zingeingia nchini na kuleta madhara. Amesema mafanikio hayo yamekuja kutokana na Tanzania kuungana na nchi zingine duniani kuridhia na kusaini Itifaki…

Read More