Kaburi la mtoto lafukuliwa, jeneza lawekwa mlangoni mwa nyumba ya babu yake
Kyerwa. Ni tukio la kushangaza. Ndivyo unavyoweza kuelezea kile kilichotokea katika familia ya Venant Zabron (52), Mkazi wa Kahinga, Kata Bugomola, wilayani Kyerwa, Mkoa wa Kagera baada ya kaburi la mjukuu wake kufukuliwa na watu wasiojulikana. Mbali na kufukuliwa kwa kaburi hilo, watu hao walichukua jeneza lilokuwa na mwili wa mtoto huyo, Faston Innocent (1)…