Kapinga afungua kikao kazi TPDC

Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga leo Septemba 17, 2024 amefungua kikao kazi cha Menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Jijini Mwanza. Lengo la kikao hicho ni kujitathmini, kujipanga na kukumbushana masuala mbalimbali ya Taasisi, ikiwemo maelekezo mbalimbali ya Serikali ya uendeshaji wa kampuni. Amewasisitize na kuwakumbusha umuhimu wa kufanya kazi kwa…

Read More

Mashindano KNK Cup 2024 yahitimishwa Bukombe

Mashindano ya KNK CUP 2024 yaliyoandaliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Mhe .Dkt. Doto Biteko ambapo timu 246 kutoka Kata 17 za Wilaya ya Bukombe imehitishwa kwa kishindo na timu ya Chui FC kutoka Kata ya Butinzya iliibuka kidedea dhidi ya timu Nyuki FC…

Read More

Mwanzo mpya wa safari ya Doyo NLD, agusia uchu wa madaraka

Kadiri giza linavyokuwa totoro, maana yake asubuhi imekaribia. Ndivyo unavyoweza kuelezea uamuzi wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama cha ADC, Doyo Hassan Doyo kuhamia chama cha National League for Democracy (NLD) na kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu. Doyo alitimkia NLD na kupitishwa kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, zikiwa zimepita siku 69 tangu aliposhindwa kwenye nafasi…

Read More

Simulizi za jiwe ‘linaloongea’ Iringa 

Iringa. Wenyeji wa Mkoa wa Iringa huliita Gangilonga yaani Liganga Lelilonga wakimaanisha ‘Jiwe linaloongea’. Inaaminika mtawala wa zamani wa kabila la Wahehe Chifu Mnyigumba, baba yake Chifu Mkwawa alikua analitumia jiwe hilo kuzungumza na mizimu kuhusu masuala mbalimbali ya utawala wake. Hili ndilo jiwe Gangilonga linalobeba jina la kata maarufu ya Gangilonga na kufanikiwa kuua…

Read More

Uchunguzi wa watekaji, mauaji ufanyike pia Z’bar

Kwa wiki mbili sasa, mada iliyotawala vyombo vya habari, baraza na vijiwe vya mazungumzo Tanzania Bara na Visiwani ni matukio ya watu kutekwa nyara na kupotea, wengine kuteswa na miili yao kuokotwa kwenye vichaka au fukwe za bahari. Katika suala hili, tumesikia sauti za wanasiasa, taasisi za kiraia, viongozi wastaafu, wanasheria na watu mbalimbali. Vilevile,…

Read More

Nani kuibuka na ushindi uchaguzi wa Rais Marekani?

Wapigakura nchini Marekani wataenda kupiga kura Novemba 5, mwaka huu, kumchagua Rais wao anayefuata. Uchaguzi huu ulianza kama marudio ya uchaguzi wa mwaka 2020, lakini ulipinduliwa Julai wakati Rais Joe Biden alipojiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho na kumuunga mkono Makamu wa Rais, Kamala Harris. Swali kuu sasa ni je, matokeo yataleta muhula wa pili wa Donald…

Read More

Miaka 32 ya vyama vingi na anguko la Tanzania kidemokrasia

Septemba 15, mwaka huu, Tanzania iliungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Demokrasia katika kipindi ambacho wanazuoni na ripoti mbalimbali zikionyesha dosari katika misingi ya demokrasia nchini. Kwa mitazamo ya wanazuoni waliozungumza na Mwananchi, uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ndiyo ulikuwa ukomo wa safari ya demokrasia nchini, baada ya hapo, kushuhudiwa misingi…

Read More