KKKT yakemea matukio ya utekaji, mauaji
Mwanga. Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) limeungana na makundi mbalimbali ya Watanzania kulaani matukio ya mauaji na utekaji yaliyotokea nchini, huku likiitisha maombi maalumu ya kuondokana na hali hiyo. Wito huo umetolewa na Mkuu wa KKKT, Dk Alex Malasusa leo Jumanne Septemba 17, 2024 wakati akitoa salamu za kanisa katika ibada ya maziko…