Mwanaume wa Kifaransa akiri “mimi ni mbakaji” – DW – 17.09.2024
Mwanamume wa Kifaransa mwenye umri wa miaka 71 amekiri mahakamani Jumanne kwamba alimnywesha mke wake wa wakati huo dawa za kulevya na kuwaalika wanaume kadhaa kumbaka kwa takriban muongo mmoja, pamoja na kumbaka yeye mwenyewe. Alimuomba yeye, na watoto wao watatu, msamaha. “Leo nasisitiza kwamba, pamoja na wanaume wengine hapa, mimi ni mbakaji”, Dominique Pélicot…