September 2024
KenGold yaendelea kutepeta, KMC yavuna pointi 3 Ligi Kuu
TIMU ya KenGold imeendeleza mwenendo mbaya wa matokeo ya Ligi Kuu Bara msimu huu baada ya kuchapwa bao 1-0 na KMC katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa KMC Mwenge jijini Dar es Salaam, ikiwa ni kichapo cha tatu mfululizo kwa kikosi hicho. Bao la KMC limefungwa na nyota wa kikosi hicho, Redemtus Mussa katika dakika…
Scholz azuru Kazakhstan kuimarisha biashara, ugavi wa mafuta – DW – 16.09.2024
Wakati wa ziara yake, Kansela Scholz amekutana na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev huko Astana. Viongozi hao wawili walionyesha dhamira yao ya kuimarisha uhusiano wa pande mbili na kusaini makubaliano ya kuongeza kiwango cha mafuta ya Kazakhstan yanayouzwa nchini Ujerumani. Taifa hilo la Asia ya Kati kwa sasa linachangia takriban 11.7% ya mafuta yanayouzwa nchini…
DC Mwanga aeleza maneno ya mwisho ya Askofu Sendoro
Mwanga/Dodoma. Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Mwanahamis Munkunda, amesimulia mazungumzo ya mwisho kati yake na Askofu Chediel Sendoro kabla ya kifo chake. Amesema katika mazungumzo hayo, Askofu Sendoro alimshauri akachukue familia yake na ailete Mwanga ili waweze kupanga namna bora ya kuwatumikia wananchi wa Mwanga. Munkunda amesema kauli hiyo ya Askofu ilikuwa ni ishara ya…
RAIS SAMIA AWASILI MKOANI KILIMANJARO,KUFUNGA MKUTANO MKUU WA MAAFISA WAKUU WAANDAMIZI JESHI LA POLISI NA MAADHIMISHO YA MIAKA 60
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili mkoani Kilimanjaro, leo tarehe 16 Septemba, 2024. Rais Dkt. Samia anatazamiwa kuwa mgeni rasmi katika kufunga Mkutano Mkuu wa Maafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi…
Kocha Ken Gold: Nakwenda kujitathimini
Wakati Ken Gold ikipokea kipigo Cha tatu kwa kupoteza bao 1-0, kocha wa timu hiyo, Fikiri Elias anafikiria kuachia ngazi kuifundisha. Fikiri ametangaza hilo leo baada ya mchezo wa ugenini wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC kumalizika, huku timu yake ikiendelea kusotea ushindi wa kwanza. Kocha huyo aliyasema hayo wakati akihojiwa na Azam TV,…
Bashe apongeza kazi nzuri za ASA Nzega
Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe (Mb) ameridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) kufuatia ziara yake ya ukaguzi wa shamba la mbegu Septemba 16, 2024 lililopo Undomo, Wilaya ya Nzega. Shamba hilo lina ukubwa wa hekta 802.47 ambapo hekta 602 zimetumika kwa ajili ya uzalishaji…
Urusi yatoa wito kwa UN na ICRC kukataa mwaliko wa Ukraine – DW – 16.09.2024
Msemaji wa Kremlin Dmitri Peskov amesema leo kwamba wanatarajia kuwa kauli kama hizo za uchochezi za Ukraine hazitakubaliwa na wahusika. Ukraine yaitaka UN na ICRC kuthibitisha hali katika maeneo ya Kursk Hii leo, Ukraine iliutaka Umoja huo wa Mataifa na Kamati ya Kimataifa ya Shirika la Msalaba Mwekundu ICRC kuthibitisha hali katika maeneo ya Kursk nchini…
Kilwa, Ruangwa waomba kujengewa daraja lililosombwa na mafuriko
Kilwa. Wanachi wanaoishi katika Wilaya za Kilwa na Ruangwa wameiomba Serikali kuwasaidia kurejesha mawasiliano ya miundombinu ya daraja la Mto Mbwemkuru linalounganisha wilaya hizo lililoathiriwa na mvua kubwa zilizonyesha mkoani Lindi. Akizungumza jana Septemba 15, 2024 wakati Naibu Waziri wa Ujenzi, Godfrey Kasekenya alipotembelea madaraja yaliyoathiriwa na mvua hizo mkoani Lindi, mkazi wa Ruangwa, Abdallah…
Rais Samia Mgeni Rasmi kilele cha Miaka 60 ya Jeshi la Polisi.
Na Mwandishi wetu Jeshi la Polisi-Moshi Kilimanjaro. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na amiri jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Daktari Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Kilele cha Miaka 60 ya Jeshi la Polisi inayofanyika katika shule ya Polisi Tanzania Moshi Mkoani Kilimanjaro septemba 17,2024. Akitoa taarifa hiyo…