Tabasamu la matumaini limerejea usoni mwa Mdamu
NYOTA wa zamani wa Polisi Tanzania, Gerald Mathias Mdamu tabasamu la matumaini limerejea usoni mwake baada ya juzi Ijumaa kufanyiwa upasuaji na kushukuru kwa kila aliyechangia kufanikisha matibabu hayo kwa kusema ‘Ahsanteni sana’. Mdamu ametoa kauli hiyo akiwa bado amelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akisubiri kutengemaa kwa afya yake ili kurudi kwenye shughuli zake…