Sudan Kusini yaahirisha uchaguzi wake Desemba, sasa kufanyika 2026
Juba. Serikali ya Sudan Kusini imetangaza kuusogeza mbele uchaguzi wake mkuu uliopangwa kufanyika Desemba 2024, hadi Desemba 2026 huku sababu kuu ikitajwa kuwa ni kutofanyika kwa maandalizi. Awali, uchaguzi huo ulipaswa kufanyika Desemba 22, 2024, lakini umeahirishwa tena ikiwa ni mara ya pili kuahirishwa. Hata hivyo, Ofisi ya Rais Salva Kiir imesema kuna changamoto zinazoukabili…