Dk Mpango aguswa na gharama upandikizaji mimba
Dar es Salaam. Makamu wa Rais Dk Philip Mpango amemuagiza Waziri wa Afya, Jenista Mhagama kuzungumza na Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba kuhusu msamaha wa kodi wa vifaa vya kupandikiza mimba, ili kupunguza gharama za matibabu kwa wananchi. “Nimepata mapendekezo ya msamaha wa kodi kwenye vifaa muhimu katika upandikizaji mimba ili kusaidia kushusha gharama…