Bosi TRA azikomalia taasisi za Serikali kulipa kodi
Dar es Salaam. Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Mwenda amesema katika uongozi wake ndani ya mamlaka hiyo, taasisi za Serikali zinazostahili kulipa kodi zisitarajie kupata upendeleo. Amesisitiza msimamo wake huo, akieleza kuwa anazichukulia taasisi hizo kama walipakodi wengine na hata zinapofika TRA, zijione na hadhi ya mlipakodi na si vinginevyo. Amesema…