
Simulizi bibi wa miaka 70 alivyofariki dunia kwa kunyweshwa dawa ya ‘Kamchape’
Katavi. Mwanamke mwenye miaka (70), Busula Andrew Magimbi Mkazi wa Kijiji cha Kaparamsenga, Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi amefariki dunia baada ya kulazimishwa na mganga maarufu ‘Kamchape’ anywe dawa ya kienyeji kwa lengo la kuondoa uchawi nyumbani kwake. Tukio hilo limetokea jana Jumatano saa mbili usiku, ambapo inadaiwa watu watatu walifika nyumbani kwa bibi huyo,…