
Miili zaidi yaopolewa Ziwa Victoria ajali ya kuzama mtumbwi
Mwanza. Miili mingine minane imeopolewa Ziwa Victoria baada ya mtumbwi wa mizigo uliobeba abiria wanaodaiwa kufikia 31 kuzama Septemba 25, 2024. Awali, Jeshi la Polisi lilisema lilikuwa likiendelea kutafuta mwili mmoja lakini imeopolewa minane, hivyo kuacha maswali kuhusu idadi ya waliokuwa kwenye mtumbwi huo. Ajali hiyo ilitokea saa 11.00 jioni katika mwalo wa Bwiru wilayani…