
Mido Coastal Union aukubali mziki wa Aucho
KIUNGO wa Coastal Union, Gift Abubakar amesema, mchezaji anayemvutia katika Ligi Kuu Bara ni kiungo nyota wa Yanga, Khalid Aucho. Gift aliyejiunga na kikosi hicho msimu huu akitokea Proline FC ya kwao Uganda alisema licha ya Aucho kutoka taifa moja ni miongoni mwa viungo bora anaovutiwa na uwezo wake, huku akiweka wazi alipotua nchini aliwasiliana…