Kagera Sugar yatambia rekodi kwa Tabora United

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Paul Nkata, raia wa Uganda amesema baada ya kucheza michezo miwili ya ligi na kupoteza yote, sasa wamejipanga kupambana kufa au kupona ili kuanza kukusanya pointi huku akiamini kwamba rekodi ya msimu uliopita itawabeba dhidi ya Tabora United. Kauli ya kocha huyo imekuja ikiwa kesho Jumatano anatarajia kukiongoza kikosi chake…

Read More

DCEA yakamata skanka kilo 1,815

Na Mwandishi Wetu Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imewakamata watu watano kwa tuhuma ya kukutwa na dawa za kulevya kilogramu 1,815 aina ya skanka ambayo ni aina bangi ya kusindika yenye kiwango kikubwa cha kemikali yenye sumu aina ya Tetrahydrocannabinol (THC). Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 10, 2024…

Read More

Vita vya Gaza ni “janga” – DW – 10.09.2024

Mkuu huyo wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya ametoa wito wa kuimarisha ushirikiano kati ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa nchi za kiarabu katika kushughulikia mzozo huo na kusisitiza kuwa mzozo huo hauna mstakabali ulio mwema: “Umoja wa Ulaya umeunga mkono kikamilifu juhudi zinazoendelea za Misri, Qatar na Marekani. Lakini makubaliano ya kusitisha…

Read More

Mmoja adaiwa kufariki dunia kwa kipindupindu Kilindi

Kilindi. Mkuu wa Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, Hashim Mgandilwa amesema mtu mmoja amepoteza maisha kwa ugonjwa wa kipindupindu huku wengine 16 wakiambukizwa ugonjwa huo wilayani mwake. Hata hivyo, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi, Mariam Mgwere alipotafutwa  na Mwananchi kuzungumzia ugonjwa huo, amesema hana mamlaka ya kuzungumzia suala hilo, badala yake akaelekeza…

Read More

Kesi ya wanandoa yaahirishwa tena, shahidi apewa amri kuendelea kufika mahakami

Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imeahirisha kusikiliza kesi inayowakabili wanandoa wawili, Bharat Nathwan na Sangita Bharat, kutokana na mmoja wa watuhumiwa ambaye ni Sangita kuwa mgonjwa, hivyo kuachwa apiganie afya yake kwanza. Akiwakilisha ombi la kuahirishwa kwa kesi hiyo, Wakili wa Upande wa Utetezi, Edward Chuwa…

Read More

ZRA yaanza hamasa ulipaji kodi kwa hiari kukusanya Sh845 bilioni

Unguja. Wakati Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) ikipanga kukusanya Sh845 bilioni mwaka wa fedha 2024/25, imeanza kuwatembelea walipakodi, kusikiliza changamoto zao na kuwakumbusha kuendelea kulipa kodi kwa hiari ili kuiwezesha Serikali kutoa huduma bora. Kaimu Kamishna Mkuu wa ZRA, Said Ali Mohamed amefanya ziara katika maeneo mbalimbali ya walipakodi kwa nyakati tofauti katika mikoa ya…

Read More