
Utata kifo kada wa Chadema
Dar es Salaam. “Ni utata mtupu,” ndiyo maneno yanayoakisi tukio la kuuawa kwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Chadema, Ally Kibao lililotokea siku moja baada ya kukamatwa akiwa kwenye basi kwenda nyumbani kwao mkoani Tanga. Kinachojenga msingi wa utata ni mazingira ya kukamatwa kwake kulikofanyika Tegeta, mbele ya Jengo la Kibo Complex, jijini Dar es Salaam na watu…