
TMA yaeleza chanzo mvua zinazoendelea kunyesha nchini
Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua zinazoendelea kunyesha kwenye maeneo mbalimbali nchini hivi sasa ni za nje ya msimu ambazo zinasababishwa na upepo unaotoka baharini. Imesema mvua za msimu wa vuli bado hazijaanza na zitaanza mwanzoni mwa Oktoba hadi Desemba 2024 huku zikitarajiwa kuwa za wastani na chini ya…