
Tarura yataja vipaumbele ujenzi wa barabara, matumizi ya teknolojia mpya
Dar es Salaam. Wakala ya Barabara Vijijini na Mijini (Tarura) umetaja vipaumbele vinne katika utendaji wao, ikiwemo kutumia teknolojia zinazohusisha kutumia malighafi zinazopatikana eneo la kazi kupata ufanisi wa gharama za ujenzi. Kipaumbele kingine ni kutunza barabara zilizopo katika hali nzuri na wastani kubaki kwenye hali hiyo, ili kulinda uwekezaji ambao tayari umeshafanyika na kuondoa…