
TUONGEE KIUME: Je, mahari si sehemu ya kuchochea mfumo dume?
Moja ya vitu vinavyonitatiza linapokuja suala la ndoa ni mahari. Ni kama nywele za kichwa, zipo hapo siku zote lakini zipo kwa ajili ya kazi gani hujui. Mahari ipo miaka nenda rudi kama mila au desturi, huku idadi kubwa ya watu wanaoitekeleza wakiitafsiri kama pesa au kitu ambacho hutolewa na mwanaume kama malipo kwa familia…