
Wafunga maduka wakigoma kuuza dhahabu Benki Kuu
Geita. Wafanyabiashara wa madini katika Soko Kuu la Dhahabu Geita wamefunga maduka wakipinga uamuzi wa kutenga angalau asilimia 20 ya dhahabu inayozalishwa na kuiuzia Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Katika soko hilo, kuna zaidi ya wafanyabiashara 50 wanaonunua dhahabu, ambao wamesema hawakuhusishwa kwenye uamuzi huo wakisema kwa aina ya biashara wanayofanya inawawia vigumu kutekeleza sheria…