
Viongozi upinzani wafunguka ishu ya ‘kuungana’
Dar es Salaam. Wakati Kiongozi mstaafu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe akivichorea ramani vyama vya upinzani ili kukishinda Chama cha Mapinduzi, baadhi ya viongozi wa vyama hivyo wamesema ni wazo zuri lakini wana hofu kuhusu utekelezaji wake. Baadhi ya viongozi hao wamesema hofu hiyo inatokana na kilichojitokeza mwaka 2015 katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),…