
Ari ya kibiashara Ujerumani yashuka kwa miezi minne – DW – 24.09.2024
Ari ya biashara nchini Ujerumani imeshuka kwa mwezi wa nne mfululizo mnamo Septemba, kulingana na uchunguzi uliofanywa huku taifa hilo lenye nguvu kubwa kiuchumi barani Ulaya likijitahidi kujikwamua kutoka mdororo wa uchumi. Faharasi ya taasisi ya Ifo iliyofanya utafiti wa makampuni takribani 1,000 inaonyesha kuwa shauku ya biashara imeporomoka asilimia 85.4 kutoka 86.6 mwezi Agosti….