Kimenya aongeza idadi ya wastaafu Prisons

IDADI ya wachezaji wa Tanzania Prisons kutamani kustaafu soka imeendelea kuongezeka baada ya Salum Kimenya, kuonesha nia ya kutundika daruga ili kugeukia shughuli nyingine nje ya uwanja. Hata ya Kimenya anayemudu kucheza kama beki na winga wa kulia, imekuja baada ya Benjamin Asukile kutundika daruga tangu kumalizika msimu uliopita na kugeukia ukocha ambapo kwa sasa…

Read More

‘Bei za nishati ya kupikia vijijini ziangaliwe upya’

Dodoma. Wadau wa mazingira nchini Tanzania wameishauri Serikali, kuanzisha wakala utakaowezesha wakazi wa vijijini kupata nishati safi ya kupikia kwa gharama ya chini kama ilivyo kwa umeme. Serikali inatekeleza mkakati wa miaka 10, ulioanza mwaka 2024, unaolenga asilimia 80 ya Watanzania ifikapo mwaka 2034 wawe wanatumia nishati safi ya kupikia. Wadau hao wameyasema hayo leo…

Read More

JKU yapiga mtu 9-0 Ligi Kuu Zanzibar

WATETEZI wa Ligi Kuu Zanzibar (ZPL), JKU juzi walitoa dozi ya maana baada ya kifumua Mwenge kwa mabao 9-0 na katika mechi ya upande mmoja ya ligi hiyo, huku nyota wa timu hiyo Mudrik Abdi Shehe akiweka rekodi msimu huu kwa kufunga mabao matano pekee yake. JKU ilipata ushindi huo kwenye Uwanja wa Gombani, kisiwani…

Read More

Wadau washauri meza ya mazungumzo Polisi, Chadema

Dar es Salaam. Wadau wa demokrasia nchini wamezitaka pande mbili zinazokinzana, yaani Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Jeshi la Polisi, kuketi meza moja ili kumaliza tofauti kwa mazungumzo. Chama hicho kimesema kinataka kufanya maandamano hayo,  ili  kuishinikiza Serikali kuhakikisha wanachama wake waliopotea wanarejeshwa, wakiwa hai au wafu. Hata hivyo, Jeshi la Polisi kupitia…

Read More

Simba, Dodoma Jiji kupigwa Jamhuri

HATIMAYE Uwanja wa Jamhuri, Dodoma umerejeshwa katika orodha ya viwanja vinavyotumika kwa michezo ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2024/2025, baada ya kufanyiwa maboresho katika maeneo ambayo yalisababisha upoteze sifa zilizoainishwa kwenye kanuni na sheria za mpira wa miguu. Tamko hilo la Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ambalo lilitolewa jana, Jumapili limeifanya Dodoma Jiji…

Read More

Hatimiliki za ardhi kupunguza migogoro Tarakea

Rombo. Wakati Serikali ikitoa hatimiliki za ardhi zaidi ya 250 kwa wananchi katika mji wa Tarakea, Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, wananchi hao wameishukuru Serikali huku wakieleza kwamba itapunguza migogoro ya ardhi kwenye maeneo yao. Wakizungumza na Mwananchi leo Septemba 22, 2024, wananchi hao wamesema migogoro ya ardhi imekuwa ni kichocheo kikubwa cha matukio ya…

Read More