
Sativa atoa notisi kuwashtaki IGP, AG akidai fidia ya Sh5 bilioni
Dar es Salaam. Mfanyabiashara wa fedha za miamala, Edgar Edson Mwakabela maarufu kama Sativa, ametoa notisi ya siku 90 ya kuwashtaki Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, akidai kulipwa fidia ya Sh5 bilioni kwa maumivu ya mwili, utesaji na udhalilishaji…