
Kada CCM adaiwa kumwagiwa tindikali Moshi
Moshi. Watu wasiojulikana wanadaiwa kumvamia na kummwagia kimiminika kinachosadikiwa kuwa tindikali, kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, Idrissa Makishe. Kada huyo mkazi wa Njoro wilayani Moshi amepata majeraha usoni na mikononi na amelazwa katika Hospitali ya Mawenzi. Msemaji wa hospitali hiyo, Venna Karia, amesema Septemba 20, saa 3.00 usiku walimpokea mgonjwa huyo…