Sekiboko arudisha tabasam kwa wanafunzi wenye ulemavu Tanga

Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Tanga, Husna Sekiboko, ametoa msaada wa vitimwendo 10 vyenye thamani ya shilingi milioni 5 kwa wanafunzi wenye ulemavu katika shule tatu zilizopo Jijini Tanga.

Shule hizo ni pamoja na Shule ya Sekondari Tanga School, Hotern na Maweni Sekondari zote za jijini Tanga .

Msaada huu unalenga kuboresha usafiri wa wanafunzi hao na kusaidia katika mchakato wa kujifunza.

Sekiboko amesema kuwa msaada huo utawasaidia wanafunzi wenye ulemavu kuondokana na changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwakabiri.