
MBUNGE MTATURU AKABIDHI MASHINE YA KUDURUFU,AMSHUKURU RAIS SAMIA.
MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameshiriki Mahafali ya 65 ya Shule ya Msingi Matongo na kuwapongeza Walimu,Wazazi na Wanafunzi kwa jitihada za kupandisha ufaulu. Aidha amekabidhi Mashine ya kudurufu yenye thamani ya Sh Milioni 3 ikiwa ni ahadi aliyoitoa mwaka jana 2023 kwenye mahafali kama hayo. Akizungumza katika mahafali hayo Octoba 2,2024,Mtaturu amewahimiza Wazazi…