Zifahamu nguzo 10 za kampeni

Dodoma. Wakati mchakato kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024 ukiendelea, wagombea na wananchi wanapaswa kutambua nguzo 10 za kufanya kampeni. Uchaguzi huo ni mchakato muhimu katika demokrasia ya nchi, kwani unawawezesha wananchi kuchagua viongozi watakaowawakilisha katika ngazi za chini za utawala. Kampeni za kistaarabu ni muhimu katika kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa…

Read More

Ahukumiwa miaka mitano jela kwa jaribio kuua

Geita. Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Geita imemhukumu kifungo cha miaka mitano jela Matokeo Petro (34), mkazi wa Bukombe mkoani Geita baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la jaribio la kutaka kumuua Josephat Mhozi (51). Hukumu hiyo imetolewa leo Oktoba 2, 2024 na Jaji wa Mahakama hiyo, Athuman Matuma baada ya kuridhishwa na hoja zilizotolewa…

Read More

Kabendera atangaza kukata rufaa dhidi ya Vodacom

Dar es Salaam. Mwanahabari, Erick Kabendera ametangaza uamuzi wa kukata rufaa dhidi ya pingamizi lililozuia kuendelea kwa kesi yake anayokabiliana na Kampuni ya mtandao wa simu ya Vodacom Tanzania Ltd. Kabendera aliifungua kesi hiyo, Julai 2024, akiituhumu kampuni hiyo kuhusika na utoaji wa taarifa za mahali alipo hadi kukamatwa kwake Julai, 2019 nyumbani kwake Mbweni…

Read More

DKT NCHEMBA AISHUKURU IMF KWA KUCHANGIA MAENDELEO YA NCHI

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi wa Timu ya Wataalamu kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bw. Harris Charalambos Tsangarides, mara baada ya kufungua vikao vya majadiliano kati ya Serikali na Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), katika ukumbi…

Read More

TBA yatoa Notisi wadaiwa sugu 648

Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) umetoa notisi kwa wadaiwa sugu 648 wa kodi ya pango ya sh. bilioni 14.8 katika mikoa ya Dodoma, Mwanza, Arusha na Mara kwa lengo la kuanza kuwaondoa katika nyumba hizo. Pia TBA imepata kibali cha Namba ya Makato Deduction Code (Vote No. S4 Code No.FC7801 TBA…

Read More

Mashambulizi ya Iran yapandisha bei ya mafuta

Muda mfupi kabla ya Iran kurusha mamia ya makombora Israel usiku wa kumkia leo Oktoba 2, 2024, tayari bei ya mafuta imeshaanza kupanda. Mashambulio hayo yanakuja kufuatia vita vinavyoendelea kati ya Israel na Kundi la Hezbollah la Lebanon. Israel ilianzisha mashambulizi katika Mji wa Beirut nchini Lebanon wiki iliyopita na kusababisha mauaji ya aliyekuwa kiongozi…

Read More

Kwa nini ZRA imevuka lengo la makusanyo

Unguja. Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA), imevuka lengo la ukusanyaji mapato kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/25, kuimarika na kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi kati ya Zanzibar na Tanzania Bara vikitajwa kuwa miongoni mwa sababu. Ongezeko hilo pia limeelezwa kuchangiwa na kuimarishwa mifumo na uhusiano mzuri na walipakodi, ikiwamo kusaidia…

Read More

Upelelezi kesi waliokuwa vigogo TPA wakamilika, kusomewa maelezo yao Oktoba 15

Dar es Salaam. Serikali imepanga Oktoba 15, 2024 kuwasomea maelezo ya mashahidi na vielelezo (Commital Proceedings), aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Madeni Kipande (66) na wenzake. Hatua hiyo inatokana na upelelezi wa kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 38/2022 kukamilika. Maelezo hayo ya mashahidi na vielelezo, yanatarajia kusomwa katika Mahakama ya…

Read More

Mkaguzi kata ya Kisangura azidi kupeleka furaha kwa wananchi

Mkaguzi kata ya Kisangura Wilayani Serengeti Mkoa wa Mara Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/Insp Genuine Kimario amezidi kupeleka furaha kwa wananchi anaowahudumia katani hapo kwa kutoa viti mwendo kwa wananchi wahitaji. Mkaguzi huyo amebainisha kuwa ameendelea kutoa viti mwendo hivyo kutokana na changamoto aliyoikuta kwa wananchi anao wahudumia ambapo aliwaomba wananchi watakao guswa kuwasaidia kundi…

Read More