
Watatu washikiliwa polisi wakituhumiwa kumlawiti mjomba wao
Arusha. Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kumwingilia kinyume cha maumbile ndugu yao mwenye miaka 27 anayedaiwa kuwa na matatizo ya afya ya akili. Akizungumzia tukio hilo leo Oktoba 2, 2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amesema wanawashikilia watuhumiwa hao wenye umri kati ya miaka 35 na 55…