
Viongozi wajifunze kuchunga midomo yao
Huku maofisini tuna watu wa kila aina. Wapo wenye makuzi ya kimjinimjini na wanaoyaishi mafunzo ya wazazi wao toka kijijini. Kuna wahuni, wastaarabu, wenye hasira na wapole. Pia, tunao wachapakazi, wavivu, wakweli na wenye husda. Mtu huonekana vizuri jinsi alivyo anapochanganya tabia zilizo kwenye makundi hayo kutegemeana na mtu alipotoka, elimu yake, uzoefu wa kazi…