
Majaliwa: Serikali imetenga bilioni 20 kukopesha wenye ulemavu. Asisitiza hakuna sababu ya kumficha mtoto mwenye ulemavu.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali imetenga shilingi bilioni 20.21 kwa ajili ya watu wenye ulemavu ikiwa ni mikopo yenye masharti nafuu na isiyokuwa na riba inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri. Amesema hayo leo (Ijumaa, Oktoba 25, 2024) alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu…