
Tshisekedi apanga katiba mpya; upinzani wahisi ni njama – DW – 25.10.2024
Tshisekedi aliapishwa madarakani mwezi Januari baada ya kuchaguliwa tena kwa muhula wa pili na wa mwisho mnamo mwezi desemba. Siku ya Jumatano, alitangaza mipango ya kuangalia uwezekano wa kurekebisha katiba, akisema kuwa katiba ya sasa, iliyoridhiwa kupitia kura ya maoni mwaka 2005, haiendani na hali halisi ya sasa ya nchi. “Katiba yetu si nzuri,” Tshisekedi…