
Mawaziri wa EU wagawika kuhusu mzozo wa Mashariki ya Kati – DW – 14.10.2024
Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya wamekutana nchini Luxembourg na kushindwa kuficha tofauti zao kuhusu mzozo unaoendelea mashariki ya kati. Waziri wa mambo ya kigeni wa Luxembourg, Xavier Bettel, amesema wazi kwamba Umoja huo sasa unakosa ushawishi na kwamba kuna mgawanyiko mkubwa kati ya mawaziri hao. Katika majadiliano, baadhi ya mawaziri walilaumu…