
Baba wa aliyechoma picha ya Rais aiangukia Serikali
Mbeya. Ikiwa imepita miezi miwili tangu kutoweka kwa msanii wa uchoraji, Shadrack Chaula (24), baba yake mzazi, Yusuph Chaula (56) ameiomba Serikali kufanya uchunguzi wa kina kujua aliko mwanaye. Mzee Chaula amesema tangu kutoweka kwa kijana wake kama familia wanaishi matumbo moto, huku jitihada za za kumtafuta zikiendelea bila mafanikio. Shadrack alitoweka baada ya kuchukuliwa…