
Harris amempongeza Trump kwa njia ya simu – DW – 06.11.2024
Msaidizi mwandamizi wa Harris ambae hakutajwa jina alisema mgombea wa Democratic “amejadili na Trump umuhimu wa kukabidhiana madaraka kwa amani na kuwa rais wa Wamarekani wote.” Donald J. Trump ndiye rais mpya wa Marekani, akishinda kura za kutosha za wajumbe maalum wa majimbo (270 zinahitajika ili kushinda) kujitangazia ushindi wa uchaguzi wa 2024. Alishinda majimbo muhimu kama…