Mastraika Ligi Kuu sasa pasua kichwa, Gamondi ana kazi
Dar es Salaam. Katika msimu wa 2024/25 wa Ligi Kuu Bara, washambuliaji wa kati wa timu kubwa za Simba, Yanga, na Azam bado wanakabiliwa na changamoto ya kufumania nyavu. Hadi kufikia mzunguko wa 11 wa ligi kwa baadhi ya timu, mastraika wa timu hizo maarufu wanaonekana kusota kupata mabao, hali ambayo imezua maswali na wasiwasi…