Sh11.18 bilioni kusambaza umeme kaya 2,970 Shinyanga
Shinyanga. Kaya 2,970 katika Mkoa wa Shinyanga zinatarajia kufaidika na mradi wa umeme wenye thamani ya Sh11.18 bilioni unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Katika vitongoji 2,703 vya mkoa huo, ni vitongoji 930 pekee ambavyo tayari vina huduma ya umeme, huku vitongoji 1,773 vikiwa bado havijapata huduma hiyo. Akizungumza leo Jumatano Novemba 6, 2024,…