Latra Morogoro yasisitiza matumizi ya sheria za usalama barabarani mwisho wa mwaka
Afisa mfawidhi wa Mamlaka ya uthibiti wa usafiri ardhini (LATRA) Mkoa wa Morogoro Andrew Mlacha amesema ajali nyingi zinazotokea barabarani zinasababishwa na makosa ya kibinadamu. Mlacha amesema hayo wakati akizungumza na Madereva wa kampuni ya Abood wakati wakipatiwa mafunzo maalum ya kukumbushwa kutii na kufuata Sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zisizo za lazima….