Benki ya Dunia yaridhisha maradi wa HEET chuo Kikuu Mzumbe
Benki ya Dunia imeonesha kuridhishwa na hatua za utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa majengo ya kisasa pamoja na kituo cha kuendeleza ubunifu (incubation center) katika Chuo Kikuu Mzumbe. Mradi huu, unaogharimu shilingi bilioni 13.2, unalenga kusaidia kukuza elimu ya juu kwa kuongeza fursa za udahili na kuboresha mazingira ya kufundisha na kujifunza chuoni hapo….