
Simulizi ya ‘Boni Yai’ alivyopata taarifa ya ushindi gerezani
Dar es Salaam. Boniface Jacob, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, ameelezea safari yake ya kipekee kuelekea ushindi wa nafasi hiyo huku akiwa gerezani, baada ya kukamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya mtandaoni. Kupitia mahojiano maalumu na Mwananchi, Jacob, maarufu kama Boni Yai, amesimulia changamoto na maamuzi magumu aliyofanya ili kuiruhusu Chadema Kanda ya Pwani kuendelea…