Dar es Salaam. Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linamshikilia Vincent Masawe, bwana harusi aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha, likieleza anatuhumiwa kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 17, 2024 Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Jumanne Muliro amesema Vincent alikamatwa kwa mganga wa kienyeji, Khamis Khalid wa Chake Chake Pemba.
Vincent alitoweka Novemba 18, siku moja baada ya kufunga ndoa jijini Dar es Salaam.
Kamanda Muliro amesema Vincent anadaiwa kuuza gari aliloazima kwa ajili ya shughuli za harusi kwa Sh9 milioni na kisha kwenda kujificha kisiwani Pemba.
“Baada ya kupatikana na kuhojiwa kwa kina alibainika kuwa na madeni mengi ambayo alijipatia kabla ya harusi na shughuli zake kutoka kwa watu mbalimbali,” amesema.
Endelea kufuatilia Mwananchi.