
Russia yafanya mashambulizi ya “kinyama” Krismas – DW – 26.12.2024
Russia ilishambulia mfumo wa nishati wa Ukraine na baadhi ya miji siku ya Jumatano kwa makombora ya masafa marefu na makombora ya balistiki pamoja na droni, katika kile ambacho Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy alikilaani kama shambulizi “lisilo la kibinadamu” siku ya Krismasi. Karibu miaka mitatu tangu vita kuanza, mashambulizi hayo yaliwajeruhi watu wasiopungua sita…