Miili sita waliofariki kwa ajali Rombo yatambuliwa

Rombo. Miili sita kati ya tisa ya watu waliofariki kwa ajali ya gari iliyohusisha basi la abiria la Ngasere na Toyota Noah, katika eneo la Tarakea katika Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro imetambuliwa huku mingine mitatu ikiwa bado haijatambuliwa. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema ajali…

Read More

Utitiri wa Wachina kila kona ni fursa au janga?

Takwimu zikionyesha kuwa China ndiyo mbia namba moja wa biashara na uwekezaji nchini, kumekuwa na mchanganyiko wa mawazo juu ya wingi wa raia Taifa hilo namba mbili kwa uchumi duniani. Wapo wanaoona wingi wa Wachina nchini ni fursa ya maendeleo kwa kuongeza shughuli za kiuchumi na wengine wakihofu kuibuka kwa unyonyaji mpya wa uchumi na…

Read More

Wakazi wa Ngombo walalama Serikali kuwahamisha bila kuwapatia maeneo

Malinyi. Wanakijiji wa Ngombo, wilayani Malinyi mkoani Morogoro wameilalamikia Serikali kwa kuanzisha oparesheni ya kuwaondoa katika kijiji hicho kupisha Pori la Akiba la Kilombero, bila kuwapatia eneo mbadala la kuhamia. Wanakijiji hao, walioko katikati ya Bonde la Kilombero, wamekubali kuondoka lakini wanahoji; wataenda wapi? Mkazi wa kijiji hicho, David Mkumba amesema alizaliwa Ngombo, na wazazi…

Read More

Taifa Stars uhakika Afcon, Guinea yaangukia pua CAF

Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) imetupilia mbali rufaa ya Guinea dhidi ya Tanzania na hivyo kuipa uhakika Taifa Stars kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon 2025) nchini Morocco. Guinea ilikata rufaa hiyo baada ya mchezo namba 143 wa kuwania kufuzu Afcon baina yao na Tanzania uliochezwa katika Uwanja…

Read More

Auawa akidaiwa kuchomwa kisu, amani yatawala Krismasi

Dar/ Mikoani. Wakati Watanzania wakiungana na Wakristo duniani kote kuadhimisha Sikukuu ya Krismasi hali ya amani imetawala nchini jana, huku tukio la mauaji ya mfugaji na mkazi wa Lubungo wa Mvomero mkoani Morogoro, Elisha Lengai (20) likitia doa. Lengai anadaiwa kuchomwa kisu na Sikonye Kipondo (22) baada ya kutokea ugomvi ambao chanzo chake bado hakijafahamika….

Read More

Desemba ya ajali, wengine 20 wafa Rombo, Tanga

Handeni. Unaweza kusema Desemba hii ni ya majonzi na simanzi kubwa kutokana na mfululizo wa ajali mbaya zilizotokea, zikiwamo zilizotokea jana wilayani Handeni Mkoa wa Tanga na nyingine iliyotokea leo Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro ambazo zimesababisha vifo vya watu 20. Mwezi huu ambao kwa kawaida huwa wa shamrashamra za sikukuu za mwisho wa mwaka,…

Read More

Utata mauaji ya mtoto wa mfanyabiashara maarufu Dom, azikwa

Dodoma. Utata umegubika tukio la mauaji ya Graison Kenyenye (6), mtoto wa mfanyabiashara maarufu wa jijini Dodoma, Zainab Shaban maarufu  Jojo. Graison aliuawa usiku wa kuamkia juzi, wakati mama yake alipokwenda matembezini na rafiki yake wa kiume. Tukio hilo lilitokea Ilazo Extension jijini Dodoma, usiku wa kuamkia Desemba 25, 2024, wakati Jojo alipomuacha mtoto huyo…

Read More