
Msimlaumu mtu! Ramovic ahitaji majembe sita, hawa wako hatarini
BAADA ya kufanyika tathimini ya washambuliaji wa Yanga kile walichokifanya msimu huu hadi sasa dirisha dogo limefunguliwa, ni wazi uamuzi unaokwenda kufanyika katika eneo hilo hautakuwa na lawama yoyote ile. Tangu ujio wa Kocha Sead Ramovic aliyetambulishwa kikosini hapo Novemba 15 mwaka huu kuchukua nafasi ya Miguel Gamondi, kumekuwa na majadiliano makubwa ya kuboresha kikosini…