Bashungwa aipa Nida siku 60 kugawa vitambulisho milioni 1.2

Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa ametoa miezi miwili kwa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) kuhakikisha vitambulisho milioni 1.2 ambavyo tayari vimeshatengenezwa vinasambazwa na kuwafikia wananchi. Waziri Bashungwa amesema hayo leo Desemba 17, 2024 jijini Dar es Salaam katika ziara ya kikazi ya kutembelea na kujionea utendaji wa…

Read More

Mwelekeo usikilizwaji kesi ya mauaji wabadilishwa

Dar es Salaam. Kesi ya mauaji inayomkabili mama anayedaiwa kumuua binti yake akishirikiana na kijana wake wa kiume imerejeshwa Mahakama Kuu ipangiwe jaji wa kuisikiliza. Awali ilipangwa kusikilizwa na hakimu mkazi mwenye mamlaka ya ziada. Washtakiwa katika kesi hiyo, Alphonce Magombola na mama yake mzazi Sophia Mwenda, wanakabiliwa na shitaka la mauaji ya mwanafamilia Beatrice…

Read More

Watano kizimbani wakidaiwa kuhujumu miundombinu SGR

Kibaha. Watu watano wakiwemo raia wa kigeni wamefikishwa mahakamani mkoani Pwani wakikabiliwa na mashItaka ya kuhujumu miundombinu ya reli ya kisasa (SGR) na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh200 milioni. Waliofikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kibaha leo Desemba 17, 2024 ni Zhang Feng, Wang Yong, Paulo John, Abdul Mohamed na Pius Kitulya, wakazi…

Read More

Bashe aingilia kati bei ya mbegu

Dodoma. Waziri wa Kilimo,  Hussein Bashe ametoa saa 24 kwa wazalishaji wa mbegu nchini kuwasilisha gharama za uzalishaji wa mbegu kwenye Taasisi ya uthibiti wa ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI) na atakayekaidi agizo hilo atafutiwa kibali cha kuzalisha mbegu.  Aidha amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa TOSCI, Patrick Ngwediagi kuhakikisha wazalishaji hao wa mbegu wanafanya hivyo vinginevyo…

Read More

WATAALAMU WA UNUNUZI WASISITIZWA UADILIFU

Na. Ramadhani Kissimba na Asia Singano, WF – Arusha Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo mbalimbali inayosimamia kada ya Ununuzi na Ugavi nchini. Akizungumza katika ufunguzi wa kongamano la 15 la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi nchini linalofanyika katika Ukumbi wa…

Read More

Alassane Diao arejea Azam na bao baada ya miezi tisa

MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Alassane Diao, amerejea kwenye kikosi hicho kwa kufunga bao baada ya kukosekana uwanjani kwa takribani miezi tisa. Diao raia wa Senegal, tangu Machi 2024 alipofanyiwa upasuaji wa goti kufuatia majeraha yake ya Anterior Cruciate Ligament (ACL), hakuonekana uwanjani mpaka leo Desemba 17, 2024 alipoingia dakika ya 81 kuchukua nafasi ya Jibril…

Read More

Air France yarejesha huduma zake KIA baada ya miaka 28

Hai. Wakati idadi ya watalii wanaoingia nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ikiongezeka kutoka 900,000 hadi milioni moja, Shirika la Ndege la Ufaransa (Air France) limerejesha huduma zake katika uwanja huo baada ya kusitisha kwa miaka 28. Hayo yameelezwa leo Jumanne Desemba 17, 2024 na Mkurugenzi wa Uwanja wa KIA, Rehema…

Read More