Kifo cha kijana aliyepigwa fimbo chaacha somo Ulanga

Ulanga. Zikiwa zimepita siku nne tangu mfugaji wa jamii ya kisukuma, Jisandu Mihayo (24) kufariki dunia kwa kinachodaiwa kupigwa fimbo kichwani, mjomba wa marehemu, Donald Paul maarufu, Trump amesema kifo cha kijana wao ni fundisho kwa jamii hiyo ambayo imekuwa ikifanya mchezo swa kuchapana fimbo. Taarifa kutoka Jeshi la Polisi zinadai kuwa Mihayo alifariki dunia…

Read More

John Tendwa aacha alama ya ujasiri

Dodoma. Kifo cha John Tendwa, msajili mstaafu wa vyama vya siasa, kimeibua kumbukumbu mbalimbali za utendaji wake uliojaa mambo mengi, ukiwepo ujasiri. Kwa mujibu wa mwanaye William, Tendwa aliyeitumikia ofisi ya msajili kwa miaka 13 amefariki dunia saa nane usiku wa kuamkia leo Desemba 17, 2024 akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa MuhimbilI (MNH). Mbali…

Read More

WATUHUMIWA WATANO, WAKIWEMO WACHINA WAWILI WANAODAIWA KUHUJUMU MIUNDOMBINU YA RELI SGR WAPANDISHWA MAHAKAMANI.

  Na Mwamvua Mwinyi, Pwani Desemba 17, 2024 Watuhumiwa watano, wakiwemo raia wawili wa China, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kibaha na kusomewa mashtaka matano ya uhujumu mali za Shirika la Reli Tanzania (TRC), na kusababisha Serikali hasara ya zaidi ya shilingi milioni 200. Watuhumiwa hao ni Zhang Feng, Wang Yong, Paulo…

Read More

Raha, karaha twisheni msimu wa likizo

Katika mfumo wa elimu wa sasa, suala la twisheni wakati wa likizo, limezua mjadala mzito nchini Tanzania, huku wadau mbalimbali wakitofautiana kuhusu umuhimu wa muda huu kwa watoto. Ingawa likizo inapaswa kuwa fursa ya watoto kupumzika na kushiriki shughuli za kijamii, baadhi ya shule zimeonekana kukosolewa na mamlaka kutokana na ufaulu duni wa wanafunzi, hali…

Read More

PPAA YAOKOA BILIONI 583 MICHAKATO YA ZABUNI ZA UMMA

Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imefanikiwa kuzuia upotevu wa fedha za serikali takribani TZS: 583,591,615,609.00 katika mshauri 162 yaliyokuwa katika hatua mbalimbali za michakato ya ununuzi wa umma kwa kipindi cha miaka takribani miaka minne. Hayo yamebainishwa na Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando alipozungumza na waandishi wa Habari pembezoni mwa…

Read More

Asilimia 10 watoto njiti wanaofika KCMC huwa katika hatari ya kifo

Moshi. Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya KCMC, Profesa Gileard Masenga amesema asilimia 10 ya watoto njiti wanaofikishwa hospitalini hapo hufika wakiwa na joto la mwili lililoshuka, hali inayohatarisha usalama wa maisha yao. Hayo ameyasema leo Jumanne, Desemba 17, 2024  wakati wa kupokea vifaa maalumu vya kufuatilia mwenendo wa hali ya watoto njiti wanapokuwa wagonjwa, vilivyotolewa…

Read More

CCM Katavi yapiga marufuku makada kujipitisha majimboni

Katavi. Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi, kimewaonya makada wake walioanza harakati hizo mapema kinyume na taratibu za chama hicho. Kwa mujibu wa duru za ndani ya chama hicho, Mkoa wa Katavi wenye majimbo matano ya uchaguzi, wamejitokeza zaidi ya makada 30 ambao wameanza kupitapita majimboni, jambo linalowapa presha wabunge walio madarakani. Akizungumza na…

Read More

DC Kilakala: Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

Morogoro. Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Musa Kilakala amesema mtu yeyote atakayekamatwa akihujumu miundombinu ya reli, barabara, umeme ama maji hatua kali zitachukuliwa dhidi yake. Kilakala ametoa kauli hiyo leo Jumanne, Desemba 17, 2024, kufuatia taarifa za kuongezeka kwa matukio ya wizi wa miundombinu, akisisitiza kuwa Jeshi la Polisi pamoja na vyombo vingine vya ulinzi…

Read More