
Kipyenga chalia Chadema, Mnyika awaonya wagombea
Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimefungua pazia la uchukuaji na urejeshaji fomu za uchaguzi wa viongozi wa wakuu wa cha hicho ngazi ya Taifa na mabaraza yake. Hatua hiyo inakwenda kuongeza joto la uchaguzi ndani ya Chadema, ambapo tayari makamu mwenyekiti wake-Bara, Tundu Lissu ametangaza nia ya kuwania nafasi ya uenyekiti….