
Gomez kuliamsha Chamazi | Mwanaspoti
MSHAMBULIAJI wa Fountain Gate, Seleman Mwalimu ‘Gomez’ huenda akauwahi mchezo wa keshokutwa Jumanne kati ya timu hiyo na Azam FC kwenye Uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamazi Dar es Salaam, baada ya kukosekana michezo miwili mfululizo iliyopita kutokana na kusumbuliwa na majeraha. Nyota huyo mwenye mabao sita ya Ligi Kuu ameng’olewa kilele cha wafungaji na…