Mbaroni akidaiwa kuiba mtoto wa miezi miwili

Mbeya. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Anna Mwakilima (24) mkazi wa Kijiji cha Mbuyuni Wilaya ya Mbarali kwa tuhuma za wizi wa mtoto wa miezi miwili, Juliana Kiwero. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga akizungumza leo Jumapili Desemba 29, 2024 ofisini kwake, amesema tukio hilo lilitokea Desemba 22, 2024 na mtuhumiwa…

Read More

Ruto aahidi kukomesha utekaji Kenya 

Kenya. Wakati vit3ndo vya utekaji raia vikikithiri nchini Kenya Rais wa nchi hiyo, William Ruto ameahidi kukomesha vitendo hivyo vilivyolaaniwa na makundi ya kutetea haki za binadamu na wanasiasa. Kwa mujibu wa tovuti ya Deutsche Welle, Sauti ya America (VOA) na Tuko, vyombo vya usalama nchini humo vimekuwa vikituhumiwa kuwashikilia wakosoaji wa serikali kinyume cha…

Read More

Utata kifo cha Wakili Manyara

Arusha. Wakati Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kikitoa tamko la kulaani kushambuliwa na kuuawa kwa Wakili Joseph Masanja, Wakili Peter Madeleka amesema ni wakati wa TLS kutumia sheria ya uchunguzi wa vifo vyenye utata kujua chanzo cha kifo hicho na kukomesha vitendo hivyo. Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Ahmed Makarani alipotafutwa na…

Read More

Nida kuwafikia wasiochukua vitambulisho kidijitali

Dar es Salaam. Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), imeanza kufanya mazungumzo na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kuja na mfumo wa kidijitali ili kuwafikishia vitambulisho Watanzania milioni 1.2 ambao hajavichukua. Wakati hatua hizo zikichukuliwa, tayari Nida imeanza kuvikusanya vitambulisho ambavyo havijachukuliwa kwa wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam na kuandaa utaratibu wa…

Read More

MBUNGE MAVUNDE PAMOJA NA TAASISI YA DODOMA LEGENDS WATEMBELEA GEREZA KUU ISANGA DODOMA

▪️Washiriki Bonanza la Michezo na Askari Magereza ▪️Watoa misaada mbalimbali kwa wafungwa ▪️Wafanya ukarabati wa Jiko lqchakula kwa Wafungwa wanawake ▪️Jeshi la Magereza lapongezwa kwa matumizi ya Nishati Safi 📍Dodoma Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde, ametembelea Gereza Kuu Isanga akiambatana na wadau wa maendeleo Dodoma, maarufu kama ‘Dodoma Legends’ jana Desemba…

Read More

Gamondi aikaushia AS FAR, aibukia Raja

MIGUEL Gamondi, aliyewahi kuinoa Yanga na kujizolea sifa kibao kwa mafanikio aliyoyapata akiwa na timu hiyo, inadaiwa ameikaushia ofa aliyopewa na AS Far Rabat ya Morocco na kukubali kutua kwa Mabingwa wa nchi hiyo, Raja Club Athletic. Awali, kulikuwa na uvumi AS FAR ilikuwa inataka kumleta Gamondi kama Mkurugenzi wa Michezo, nafasi ya kiutawala ambayo…

Read More

Mwaka 2024 unavyoacha huzuni katika sekta ya anga

Dodoma. Ajali ya ndege ya Jeju Air, Boeing 737-800 iliyotokea jana Korea Kusini na kusababisha vifo vya watu 179, huku wahudumu wawili wa ndege hiyo wakinusurika kifo, imefunga mwaka kwa kuwa ajali ya ndege iliyoua watu wengi zaidi mwaka 2024. Ajali nyingine za ndege zilizoua watu wengi ni iliyotokea Desemba 25, 2024, ambapo ndege ya…

Read More

Maimuna akiri Misri mziki mnene

KIUNGO wa Zed FC, Mtanzania Maimuna Hamis ‘Mynaco’ amesema Ligi ya Misri imekuwa ngumu kiasi ambacho ukipoteza mchezo mmoja unasogea hadi nafasi ya chini. Nyota huyo amezidi kuwa na kiwango bora msimu huu na ndio kiungo tegemeo ndani ya Zed FC iliyopo nafasi ya nne kwenye msimamo. Akizungumza na Mwanaspoti, Mynaco alisema hadi sasa timu…

Read More

Othman ahimiza uwekezaji hifadhi za misitu

Unguja. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman amesema ipo haja kuwekeza katika miradi ya uhifadhi misitu ili kuongeza mapato ya Serikali kupitia utalii. Othman amesema hayo leo Jumapili Desemba 29, 2024 katika Msitu Masingini wakati akiweka jiwe la msingi la Mradi wa Utalii Rafiki na Mazingira ulioanzishwa na Jumuiya ya Zanzi Eco-…

Read More